top of page

EMANCIPATION MONTH

BRAMPTON CITY HALL

A REMINDER OF THE STRUGGLES PEOPLE OF THE BLACK COMMUNITY ENDURED TO SEEK FREEDOM

AUG 3, 2026

Emancipation Month ni kumbukumbu ya safari ya uhuru, ni sherehe ya utamaduni, na ni ahadi ya mustakabali wenye usawa. Tuendelee kusimulia hadithi zetu, kusherehekea mizizi yetu, na kupigania haki zetu – leo na kesho

Sauti za africa ilishuhudia sherehe ya kuadimisha Black History Emancipation Month. 

Sherehe hiyo ilifanyikwa City Hall Brampton kwenye ukumbi wa nje. Bendera rasmi ya Black history ilipandishwa na viongozi mbali mbali walikuwepo wakiwa miongoni mwao Diwani wa Ward 9 na 10 Mr Gurpartap Singh Toor na Diwani Rod Power. Mr. Dewitt Lee ambaye ni mkurugenzi wa Black Emancipation Tour na mwanzilishaji hapo jiji la Brampton naye alikuwepo pamoja na mke wake ambaye naye ni mwanzilishaji kwa heshima yake ya kipekee wakati  ameshika mamlaka zake miongoni mwao ikiwa kuburudisha wote tulioshuhudia na musiki wa Steel Drums aina noma kabisa!  Orodha ya watu wa kusifiwa kibinafsi ni kubwa mno na hatutaweza kuwataja wote hapo. Wengi wao wana sifa za kiwango cha juu kabisa - wengi walipotolea maisha yao katika mapambano na ubaguzi na ukandamizi dhidhi ya watu weusi pale nyuma wakati wa enzi za miaka 1800 na baadaye!

Mwezi wa Black Emancipation ni tukio muhimu, si tu kwa sababu ya uzito wake wa kihistoria, bali pia kwa sababu unatukumbusha kwa ukali umuhimu wa kupigania uhuru—na kwamba safari hii ni endelevu bila kikomo. Ingawa mafanikio makubwa yalifikiwa na wapigania uhuru wa awali na mashujaa wa aina mbalimbali, wakiwemo, lakini sio tu, Mchungaji Martin Luther King Jr., Mohammed Ali, Dkt. Jean Augustine, Bi. Rosemary Sadlier, na wengine wengi ambao ni vigumu kuwataja wote, Black Emancipation Month si tukio linaloweza kuhusishwa na mtu mmoja pekee.

Badala yake, ni harakati pana na endelevu duniani kote, inayolenga kutoa heshima na kutambua umuhimu wa kihistoria wa kuwakomboa watu wa asili ya Afrika waliokuwa watumwa. Mwezi huu unaadhimishwa ili kutafakari juu ya nguvu, ustahimilivu, na ujasiri wa jamii za watu weusi, na pia kupambana na ubaguzi wa rangi na aina mbalimbali za dhuluma zinazoendelea hadi leo.

Ni jambo la kutisha kufikiria kwamba ubaguzi wa rangi bado upo katika karne hii, na mara nyingi hujitokeza kwa sura na mbinu tofauti. Ingawa dhana ya Emancipation Day ilianzishwa nchini Kanada, tunapaswa pia kutambua kwamba utambuzi mpana wa historia ya watu weusi na mapambano dhidi ya utumwa umeundwa na juhudi za watu na mashirika mbalimbali kwa kipindi kirefu.

Umuhimu Wake Leo

  • Kuelimisha wajamii historia ya watu weusi nchini Kanada

  • Mapambano dhidi ya utumwa, ubaguzi na ukandamizaji

  • Mchango wa watu weusi katika ujenzi wa taifa

  • Nafasi ya kizazi kipya kujifunza, kutafakari, na kusherehekea utambulisho wao

Black History Month (Februari) na Emancipation Month (Agosti) ni nguzo mbili zinazounganisha historia ya uhuru na safari ya haki za binadamu kwa watu wa asili ya Afrika. Lakini zaidi ya hayo, ni ushindi wa kufungua mlango kwa watu wengi wa jamii wasiyo zaliwa binadamu mweusi. Uhuru ni kwa ajili ya sisi sote. Na mimi mwenyewe nipo katika kundi hicho.

20260803_091359.jpg

Distinguished architecture signifying the City of Brampton. Located just outside the City Hall building on city grounds.

Me Dewitt Lee with Ms. Liberty Silver preparing for the singing of Canadian National Anthem.

Mr. Dewitt Lee making a speech on Emancipation Month Act which was decreed 5 years ago.

Mr. Dewitt Lee giving historical reference to farming of Tobacco, Sugar and Coffee where illegal slave labour was imposed upon peoples of the black community

20260803_115324.jpg
With Ms. Suzette Vidale,
maestro of steel drums wo performed playing live at the event!
20260803_120144.jpg
With World Class Singer and Crooner extraordinaire Ms. Liberty Silver. Amazing baritone voice!
00:00 / 00:35
00:00 / 01:00
20260803_110108.jpg
The Black Emancipation Flag 
20260803_125545.jpg
With Mr. Dewitt Lee, founder of Black Emancipation Tour and organizer for City of Brampton 
20260803_125611.jpg

Mr Dewitt Lee with Mr. Khalid Magram, founder of Msimulizi Community news based in Toronto, Ontario. Mr Khalid Magram is also the originator (the brainchild) for Swahili Heritage Month Act in the parliament of Ontario legislature which has been forwarded through the offices of NDP MPP Kristyn Wong-Tam. The Bill has passed first reading and will be adjudicated for the second reading and receipt of the Royal Assent immediately after parliament resumes following the summer recess.

00:00 / 01:07
00:00 / 02:15
00:00 / 00:52
00:00 / 00:58
00:00 / 02:05

© 2026  by THINKBIG GROUP INTERNATIONAL. 

bottom of page